Monday, 8 September 2014

AIR BUS YAUA WANNE KATIKA AJALI ILIYOTOKEA GAIRO MOROGORO HII LEO


Ajali hiyo
Screen Shot 2014-09-08 at 2.26.41 PM
Add caption

Habari kutoka Mkoani Morogoro zinapasha kuwa basi la Kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Tabora limepata ajali mapema hii leo katika  eneo la Kiegeya Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.

Habari hizo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile.

"Ninaomba unitafute baade kidogo kwa taarifa kamili kwa sasa nipo eneo la ajali huku Gairo," alisema SACP Shilogile alipokuwa akiwasiliana na wanahabari mbalimbali.

BONGO LEAKS itakujuza zaidi kuhusiana na tukio hilo ambalo linaelezwa kugharimu uhai wa watu 4 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment