Thursday, 28 August 2014

SHULE 19 ZA SEKONDARI MUFINDI ZASHIRIKI SHINDANO LA UTOAJI HOTUBA KWA KINGEREZA

Mmoja wa wanafunzi akimwaga sera kwa kimombo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Muhagama alikuwepo
Katika picha ya pamoja na wanafunzi na wengine wengine waliohudhuria shindano hilo
Wakati wakifuatilia
Mratibu wa shindano Dickson Mseti
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama amewataka wadau wa elimu kuacha kuzibeza shule za wananchi maarufu kama shule za kata badala yake washirikiane na serikali kuziboresha ili ziwe bora.

Akizungumza kwenye mashindano ya hotuba kwa lugha ya kingereza yaliyoshirikisha wanafunzi wa shule 19 za sekondari za wilaya ya Mufindi, mjini Mafinga hivikaribuni Mhagama alisema alisema shule hizo zitafanya vizuri zaidi endapo pande zote zitaungana kuzisaidia.

“Baadhi ya watu walikuwa wanabeza juhudi za kuendeleza elimu nchini, lakini kwa kadri tunavyokwenda tumeanza kuona mafanikio ya juhudi hizo” alisema.

Akitoa mfano wa matokeo ya juhudio hizo Mhagama alisema matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yamedhihirisha mafanikio hayo.

“Wilayani yenu ya Mufindi ni ya mfano. Katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu, mmetoa shule mbili bora kati ya kumi nchini, na kati ya shule hizo mbili Igowole imeongoza kitaifa,” alisema na kuitaja shule nyingine kuwa ni Kawawa iliyoingia kumi bora.

Akizungumzia mitaala ya elimu ya sekondari, Naibu Waziri alisema serikali imeanza kulifanyia kazi suala hilo ili kuwe na mitaala itakayowawezesha wanafunzi kujitegemea baaada ya kuamaliza masomo yao tofauti na mfumo wa sasa unaowaaandaa kuajiriwa.
  
Mratibu wa mashindano ya hotuba, Mwalimu Dickson Mseti alisema mashindano hayo yaliyopewa jina la I can Think, I can Speak, yamefanyika kwa mara ya tatu wilayani humo yakiwa na lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo na ujasiri wa kujieleza mbele za watu.

Alisema mashindano haya yanatarajiwa kurudisha hadhi ya elimu kwa wanafunzi kuwa na ujasiri wa kudadavua mambo na kuyaeleza kwa kujiamini.

“Tuna wasomi, lakini wenye shida ya kujieleza, hili ni tatizo linalokua siku hadi siku, mashindano haya yanaweza kusaidaia kukabiliana na hali hiyo,” alisema.

Alisema chimbuko la mashindano hayo ni mijadala iliyobuniwa na shule ya Brooke Bond mwaka 2011 kwa lengo la kuhamasisha na kuwahimiza vijana kuwa na muono wa kuandaa kizazi kinachoweza kutoa maoni yao kwa kujiamini.

Mshindi wa kwanza kwenye mashindano hayo alikuwa Ladina Msigwa kutoka shule ya sekondari Brook Bond ambaye alizungumzia umuhimu wa wananchi kushirikishwa kwenye mchakato wa Kuandika Katiba mpya.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment