Wednesday, 27 August 2014

MCHUNGAJI MSIGWA AWATAKA MADEREVA WA BODABODA KUZINGATIA SHERIA YA LESENI YA USAFIRISHAJI

Mchungaji Msigwa akisisitiza jambo katika kikao chake na madereva wa bodaboda wa mjini Iringa
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amewataka madereva wa bodaboda wa mjini hapa kuzingatia sheria na kanuzi za usafirishaji.

Katika kikao chake alichofanya hivikaribuni na madereva hao, Mchungaji hayuko tayari kuona haki za watu wengine zinadhulumiwa ili kuwanufaisha watu wengine.

Aliyasema hayo baada ya mmoja wa madereva katika kikao hicho, Ibrahim Musa kumuomba mbunge huyo asaidie kuzipiga marufuku bajaj kupaki katika maeneo wanayopaki madereva wa bodaboda.

“Mheshimiwa mbunge katika kijiwe chetu sisi kuna pikipiki nyingi sana, cha ajabu bajaj nazo zimeruhusiwa kupaki hapo. Sasa zimeanza kutukosesha biashara kwasababu sisi gharama yetu kwa safari fupifupi za mjini ni Sh 1,000 wakati wao wanachukua Sh 500 kwa abiria mmoja,” alisema.

Alisema kiasi kinachotozwa na madereva wa bajaj kwa abiria kimewafanya wengi wao wakimbie kupanda bodaboda na hivyo kuwaathiri kimapato.

Mchungaji Msigwa alisema madereva wote wa usafirishaji ni lazima wazingatie sheria na kanuni za usafirishaji.


“Tunafahamu zipo bodaboda, zipo taxi, zipo daladala na hata maroli. Hawa wote ni watanzania, wote ni lazima wafaidi matunda ya kazi yao, pasiwepo mmoja anayenufaika zaidi,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment