Thursday, 28 August 2014

KUTOKA MABANDA YA KINYWAJI NA VIJIWE VYA IRINGA MJINI. WASIOSIKIKA HOLIDAY BAR WASEMA PINDA ANA BEEP URAIS


JANA Agosti 27 BONGO LEAKS ilitembelea banda maarufu linalouza kinywaji mjini Iringa.

Ni Holiday Bar; kwa wasio wenyeji wa mjini Iringa, Bar hii maarufu ipo Kijiweni karibu kabisa na msikiti wa Hidaya.

Ni maarufu kweli kweli na kwa mjini hapa inafananishwa na zile bar maafuru za jijini Dar es Salaam kama Corner Bar. Ni Bar inayopendwa na wateja wa rika zote labla kwasababu ya umashuhuri wake na huduma zinazojali mteja.

Wapo wanaosema umashuhuri wake na ubora wa huduma unaifanya iwe moja kati ya Bar chache za mjini Iringa ambazo mauzo yake hayatetereki.

BONGO LEAKS ilitembelea hapo na kama kawaida ikakuta wateja wamefurika lukuki, wakinywa na kucheza; kama hujawahi kufika jaribu sasa.

Nje ya banda hili kulikuwa na kundi la wateja, wadada na wanaume wakijadiliana haya na yale. BONGO LEAKS ikajiridhisha kwamba wadada hao na wababa wana sauti, lakini hazijasikika.

ASIYESIKIKA mmoja akasema………aaah hata Pinda naye anataka urais? Mbona alishawahi kutangaza kwamba atastaafu siasa baada ya serikali ya Jakaya Kikwete kumaliza muda wake.

ASIYESIKIKA mwingine akadakia…..hata mimi nimeshangaa kusikia anautaka urais, mbona hajatwambia kwamba anafuta ile kauli yake ya mwanzo tena iliyokuwa na pendekezo la ukomo wa ubunge.

Nakumbuka Mizengo Pinda aliwahi kushauri kwamba Katiba ifanyiwe marekebisho ili kuwe na ukomo kwa wanaogombea na kupata ubunge. Alishauri ziwe awamu tatu ili kutoa fursa kwa watanzania wengine kuongoza na akapigilia msumari akisema baada ya 2015 atastaafu siasa.

Leo inakuwa anasema anataka urais? ASIYESIKIKA mwingine akaohoji na kusema …..lakini nadhani PINDA ANA WA BEEP TU WAGOMBEA WENYE NGUVU, unadhani hapendi kuhabika kama ilivyokuwa kwa Sumaye. Pinda anajua NYWELE NYEUPE ndio kila kitu, huyo ndiye atakayechuana na Dokta Slaa wa Chadema 2015.

Na wakitaka kujua Nywele nyeupe anakubalika wasimamishwe mahali halafu litangazwe tangazo kwa watanzania wanaowapenda viongozi hao wakasimame nyuma yao. ASIYESIKIKA huyo akasema….naamini kila atakakokwenda Lowasa atakuwa na watu wengi.

ASIYESIKIKA mwingine akasema katika kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM wapo watu wanaoweza kumpa ushindani Lowasa na hao si wengine zaidi ya Januari Makamba na Mwigulu Nchemba.

Hao ni vijana na wapiga kura wengi ni vijana, mimi naamini wanaweza kutikisa harakati za Lowassa.

BONGO LEAKS kimyaa, haikutaka kuchangia hoja hiyo kwa hofu kwamba isijeikatafsiriwa kwamba inamfanyia fulani kampeni.


Itaendelea……………………………….  

Reactions:

0 comments:

Post a Comment