Monday, 14 July 2014

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AUMEZEA URAIS 2025

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Hamis Juma ameombea amani nchini ili ndoto yake ya kuwania urais wa Zanzibar mwaka 2025 itimie.

“Eeehh CCM inaruhusu kutangaza nia; kinachokatazwa ni kufanya kampeni kabla ya muda, wanaofanya kampeni kabla ya muda lazima watashughulikiwa,” alisema.

Sadifa alionesha nia hiyo juzi wakati akimuapisha Profesa Peter Msolla kuwa Kamanda wa UVCCM wa wilaya ya Kilolo.

Shughuli za kumwapisha Profesa Msolla ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo na Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais zilifanyika katika kijiji cha Kidabaga wilayani humo.

Alisema amani na usalama wa watanzania na mali zao sio kazi ya jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama peke yake bali ni kazi wajibu wa kila mtanzania mwenye nia njema na Taifa hili.

“Kwa uzoefu naoendelea kupata katika siasa za nchi hii naweza kabisa kuwa Rais wa Zanzibar mwaka 2025. Lakini tukikubali amani yetu ichezewe na kuifanya nchi iwe vipande vipande, ndto hiyo hawezi kuifikia,” alisema.

Alisema kila mtu katika maisha yake ya kila siku anayo ndoto au malengo yake anayotaka ayafikie katika kipindi cha muda fulani; hali hiyo itawezekana endapo kila mmoja atashiriki kwa nafasi yake kuhubiri amani na utulivu uliopo uendelee.

Alisema vipo vyama na wanasiasa wake ambao badala ya kuhubiri amani inayowafanya wawepo katika ofisi walizopo, vinawaandaa vijana kufanya machafuko.

Alisema vyama hivyo na wanasiasa wa aina hiyo hawafai hata kidogo na ni muhimu kwa watanzania wakajiepusha na hila zao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment