Tuesday, 1 July 2014

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015, JIMBO LA LUDEWA NI KATI YA DEO FILIKUNJOMBE NA DK PINDI CHANA

Deo Filikunjomba

Dk Pindi Chana
WAKATI serikali ikiwapasha wananchi wake kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Oktoba mwaka huu utategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya, mtandao huu unaendelea kukupasha heka heka za mchakato wa Uchaguzi Mkuu majimboni mwaka 2015.

Leo hii tunakuletea hekaheka za kusisimua kutoka Jimbo la Ludewa Mkoani Njombe.

Kwa mwaka wan ne sasa jimbo hilo linaongozwa na mbunge kijana Deo Filikunjombe; Filikunjombe anafahamika na watanzania wengi kwa uwezo wake wa kushawishi na kujenga hoja akiwa bungeni.

Nje ya bunge, Filikunjombe ni mbunge wa aina yake na huenda akawa mmoja kati ya wabunge wachache wa mikoa ya Njombe na Iringa aliyemudu vilivyo kutekeleza ahadi nyingi za uchaguzi alizotoa yeye mwenyewe wakati wa Uchaguzi wa 2010 na zile zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani yake ya uchaguzi.

Amefanya mengi na amesema mengi. Mtandao huu uataendelea kukujuza yale yote yaliyofanywa na yaliyosemwa na mbunge huyo katika medani ya siasa jimboni humo na Taifani kwa ujumla.

Pamoja na hayo yote Filikunjombe anakabiliwa na upinzani; ni upinzani unaolezwa kuwa mkali kutoka kwa Naibu Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Hazara Chana.

Ndio, pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalumu toka mkoa wa Njombe kwa mwaka wa tisa sasa anaoneka mwiba kwa mbunge huyo, anataka kujitosa kuwania jimbo hilo hasa baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba CCM inataka wabunge wote wa viti maalumu walioshika nafasi hizo kwa zaidi ya muhula mmoja wakajaribu majimboni kupisha wanawake wengine katika nafasi hizo za viti maalumu. Lolote linaweza kutokea katika uchaguzi huo wa 2015.

Kikubwa kinachotegemewa na Dk Pindi ni uwezo wake kisiasa; akiwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk Pindi ni mwanamama anayeheshimika sana katika medani za siasa nchini.

Lakini nafasi aliyonayo serikalini inamfanya aaminike na wapiga kura wa jimbo hilo; baadhi yao wanasema hawataki kupoteza nafasi ya waziri waliyopata kutoka kwa mwanasiasa anayetoka katika jimbo hilo, kwahiyo wanamuahidi kumpa kura zao ili kulinda heshima hiyo inayoelezwa kama fursa kubwa kwa wana Ludewa.

Pamoja na hayo yote Dk Pindi Chana na Deo Filikunjombe wanatofauti kubwa za kimtizamo na kiutendaji………endelea kusoma mtandao huu, unajipanga kukujuza zaidi

Reactions:

0 comments:

Post a Comment