Monday, 7 July 2014

HIZI NDIZO MBWEMBWE ZILIZOONESHWA NA MASTAA WA BONGO KATIKA TAMASHA LA NCHI ZA MAJAHAZI


MASTAA  wa bongo waliopata mwaliko kuhudhuria swahili day katika tamasha la nchi za majahazi walionesha vituko vya mwaka ambavyo viliacha wengi wenye utaratibu kujiuliza kulikoni. 

Wakati wakichelewa kuingia katuika tamasha, walipofika kitu cha kwanza walitaka kupewa mabodigadi na kuwaacha waandazi wa tamasha hilio katika hali ngumu ya sintofahamu.

Pamoja na kudai walinzi hao maarufu kama mabaunsa kwa kuwa wao ni mstaa na hawataki kudhurika, wengi walionekana kutojua nini hasa kimewapeleka pale kama ni umaarufu au la.

katika ukumbi wa mambo, usiku kila mtu alijua kwamba mastaa wamefika kwani waligeuza eneo hilo kuwa lokesheni kw amabusu na kukaliana.

kituko cha kuklaliana kwa wapenzi hakikulinganisha na baadhi yao kuonekana kama wanaigiza baada  ya kutaka wapatiwe ulinzi wa kampuni binafsi iliyopewa kazi ya kulinda katika tamasha hilo.

Wasanii hao walisema kwamba wanafuatwa na watu  mbalimbali waliofika eneo hilo wakitaka kupiga nao picha na hivyo usalama wao ni mdogo kitendo.

"Mimi niliona sasa si sawasawa kwani wapo mastaa wengi kutoka Ulaya wapo na hawajahitaji ulinzi wa mabaunsa" alisema ofisa mmoja wa tamasha hilo ambaye alikuwa anashughulika na kupokea wageni na kuwaelekeza wapi kwa kwenda.

Ofisa huyo alisema kwamba Mmoja wa walinzi wa kampuni ya ulinzi iliyokuwa ikilinda eneo hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake aliwaeleza  wasanii hao waliotaka ulinzi kwamba kampuni yao haijapewa taarifa za kutoa mlinzi kwa kila msanii wa filamu isipokuwa kazi yao ni kuimarisha ulinzi kwa wote walioudhuria tamasha hilo.

Kituko kingine ambacho kilielezwa na  ni kitendo cha msanii mmoja kutaka mpenzi wake alipiwe gharama zote kwani ni msanii mwenzake, ingawa huyo mpenzi hakuwa katika orodha ya waalikwa wa ZIFF ambao wanalipiwa gharama  za maisha hapo.

msanii huyo ambaye ni mwangavu na mpenzi wake mwangavu pia ndio waliokuwa wakionekana katika maeneo ya Klabu ya Mambo wakiwa wanapakatana muda wote kama kumbikumbu.
Ilikuwa kazi wakati waandazi walipokuwa wakimweleza kuwa mkataba walioingia ni wa yeye pekee na wala si pamoja na mpenzi wake.

"Kama umemleta wewe ndiwe mwenye jukumu na suala si la kuwa msanii bali nani amealikwa"

 “Hata kama hayupo katika ratiba zenu huyu naye ni msanii naye alipwe gharama kama wasanii wengina,’’ alisema  muigizaji huyo ambaye pia ni dairekta.

 Hata hivyo vituko zaidi vilionekana katika siku ya tuzo ambapo walichelewa kufika na hivyo kulazimika kujichanganya na wengine badala ya maeneo yao ya waalikwa.

Mbwembe za mastaa hao ambazo pia zilionekana katika tamasha kwa kumwaga kilaji na kutokuwa na nidhamu ya kutosha ziklizonekana pia siku ya mkutano na waandishi wa habari, wakifika wakiwa wamechelewa na mmoja wa mastaa ambaye jana yake alitaka mpenzi wake alipiwe alikacha kuhudhuria mkutano huo.

Mkutano huo uliowajumuisha waigizaji, waongoza filamu na wanamuziki kadhaa wa kimataifa, ulikuwa mchungu kwa wasanii ambao walijohi uhalali wa wao kufika mwishoni mwa tamasha huku wakiwapa elimu kuhusu umuhimu wa kuhudhuria matamasha makubwa kama hayo ili kutafuta nafasi za kufanya kazi kimataifa.

 Haji Adamu “Baba Haji” alijibu hoja ya wapi walipokuwepo, swali lililoulizwa na mwandishi kutoka Kenya alianza kwa kusema: “binafsi nilikuwa na tatizo la kuguza mama yangu huko Tanga ambaye alikuwa anaumwa, sikuweza kuja kwa wakati ili kudadavua maswali yaliyohusu filamu zangu tatu zilizoonyeshwa,” alijitetea.

mwandishi huyo wa kenya alisema lishangazwa sana na jinsiwasanii wa Tanzania walivyoshindwa kuhudhuria japo siku za skrini za filamu zao, hali iliyowamnyima watu kuuliza maswali.

Waandishi waliwashauri kwamba suala la kuigiza na kujifunza na kutafuta fursa ya soko ni muhimu, na hawana sababu za kusubiri mwaliko wa siku moja kwani hauwasaidii kitu.

Maelezo hayo yalitokana na jibu la Richie Richie kwa swali la kwanza kwamba wao hawana fedha za kuhudhuria siku zote kutokana na kutofanya vyema katika biashara.

“Kikubwa kinachotukwamisha tushindwe kuhudhuria tangu siku ya kwanza ni uwezeshaji, filamu za kitanzania jinsi ya uuzaji inashindikana, tungeweza vipi kuishi Zanzibar kwa siku 10, huku filamu tukishamuuzia Mhindi ndiyo imekula kwetu..." alisema na kusema wangelikuwa na fedha wangelikuja kuangalia.

Hali ya ukosefu wa fedha unatokana na wasanii kuwauzia wasambazaji haki zao, ilhali kuna uwezekano wa kumaliza tatizo hilo iwapo wakijituma na kutompa haki zlote msambazaji.

“Ina maana mpaka leo bado hamjajua umuhimu wa elimu? Kuhudhuria katika tamasha hili ni elimu tosha, pia mnakuwa katika nafasi nzuri ya kupata kuhamiana na wasanii wa kimataifa, ni wakati wa kujitambua tumia fedha zako mwenyewe na si kusubiri kuwezeshwa,” alisema mmoja wa waandishi wa habari.

Katika hali inayoonekana kuwa sehemu ya mwendelezo wa mbwembwe za mastaa mmojawapo alimcheka mwenzake alifuata nini chuoni wakati anashindwa kufanya vizuri katikasoko. Kwa Bongo Movie kwenda darasani ni ujinga.

Katika kuonesha tatizo la mastaa wa Bongo hata madairekta waliongiza filamu zao hawakuwepo siku ya tuzo za Kiswahili.

Kwa mfano filamu ya Shahada na dairekta wake Issa Mussa ‘Cloud 112’ walitwaa tuzo za Zuku Bongo Movie katika tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) huku filamu  ya Shikamoo Mzee ikitwaa tuzo ya wananchi.

Watengeneza sinema hizo wote wawili hawakuwepo Jacob Steven aliondoka siku ile ile asubuhi wakati Cloud hakuwepo kabisa.

Shahada ni filamu ya kidini ambayo inaelezea ni jinsi gani binadamu anapaswa kuishi katika mazingira ya kufuata misingi ya dini.

Filamu ya Shahada imeongozwa  na kuigizwa na Issa Mussa ‘Cloud 112’ wakati shikamoo mzee ilitengenezwa Jacob Steven.

Wakati tuzo za Shahada zilipokelewa na Mtitu, muigizaji shamsa Ford ndiye aliyepokea tuzo ya Shikamoo Mzee.

Aidha katika mlolongo wa tuzo Muigizaji bora wa kiume alikuwa Jackson Kabirigi kupitia sinema ya Kisate na Nguvu ya Imani huku muigizaji bora wa kike akiwa ni Esha Buheti kupitia sinema ya Mimi na Mungu wangu.
mwisho


Reactions:

0 comments:

Post a Comment