Monday, 30 June 2014

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA SAOHILL MUFINDI WAMGOMEA MWAJIRI, WADAI NYONGEZA YA MISHAHARA NA MALIMBIKIZO YAO

Mkurugenzi wa Makampuni ya GRL, Roselyne Mariki (kulia) akionesha sehemu ya mitambo ya kiwanda chao katika tukio lililofanyika siku kadhaa zilizopita
Zaidi ya wafanyakazi 200 wa Kiwanda cha Saohill kilichopo  wilayani Mufindi mkoani Iringa leo hii wamegoma kuendelea na kazi wakimshinikiza mwajiri wao kupandisha mishahar na kulipa malimbikizo ya madai yao mbalimbali.

Taarifa zilizoufikia mtandao huu zimesema, badhi ya wafanyakazi hao walikusanyika makao makuu ya kiwanda hicho, kilichopo nje kidogo ya mji wa Mafinga, ndani ya msitu wa Taifa wa Saohill, mapema asubuhi ya leo wakiwa na mabango.

Katika mabango hayo kulikuwa na ujumbe uliokuwa ukishinikiza kiwanda hicho kilichopo chini ya kampuni mama ya Green Resources Ltd kuwalipa malimbikizo na nyongeza ya mishahara yao sambamba na kuboreshewa mazingira ya kazi.

Mtandao huu unaendela kumtafuta Meneja wa kiwanda hicho aliyetajwa kwa jina moja la Mwakibinga na Mkurugenzi wa Makampuni ya GRL, Roselyne Mariki kujua hatma ya madai ya wafanyakazi hao.

Taarifa zilizotolewa na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo zimesema mgomo huo ulisitishwa majira ya saa tisa mchana baada ya uongozi wa kiwanda na ule wa Chama cha Wafanyakazi wa kiwanda hicho kuahidi kuyatolea majibu madai hayo, Jumatano ya wiki hii.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment