Tuesday, 10 June 2014

UAMUZI WA RUFAA YA WAMBURA KUTOLEWA USIKU HUU

michael wambura
WADAU na wapenzi wa klabu ya samba wanasubiri kwa hamu kubwa matokeo ya rufaa iliyokatwa na mgombea aliyewekewa pingamizi Michael Richard Wambura.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaendelea kuifanyia kazi rufani yake aliyoiwasilisha Mei 29, 2014.

Wambura aliwekewa pingamizi na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Simba,Seydou Rubeya.Rubeya amedai kuwa pingamizi lake linajikita katika hoja ya kwamba Wambura aliwahi kupeleka masuala ya soka mahakamani na pia aliwahi kufisadi TFF.

Taarifa zisizo rasmi ambazo zimetupiwa katika mtandao wa jamii forums hivi punde zinadai kwamba wambura ameshinda dhidi ya pingamizi hilo.


Taarifa hiyo ambayo hata hivyo imekanusha na mmoja wa viongozi wa TFF aliyedai kwamba kikao bado kinaendelea zinadai kwamba kwa ushindi huo, Wambura amepitishwa kugombea Urais katika club ya simba unaotegemewa kufanyika Juni 29, 2014 jijini Dar es salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment