Monday, 23 June 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII; KICHANGA CHATUPWA KATIKA KONTENA LA TAKA KARIBU NA OFISI YA MKUU WA WILAYA IRINGA

Mwili wa kichanga ukiwa katikati ya maboksi katika kontena la taka Iringa mjini

baadhi ya mashuhuda walioshuhudia tukio hilo
MWILI wa kichanga kinachoonekana kilitolewa kabla ya muda wake (abortion) umeokotwa ukiwa umetupwa katika kontena la tako lililopo jirani na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa upande mmoja na Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa upande mwingine.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,kichanga hicho kimekutwa katika kontena hilo leo asubuhi kikiwa kimefungashwa kwenye maboksi.

Baadhi ya watu walioongea na mtandao huu wameonesha masikitiko yao makubwa dhidi ya tukio hilo.

“Huwezi jua mtoto huyu kama angetunzwa vizuri hadi kuzaliwa kwake angekuwa nani katika maisha yake; kitendo kilichanywa na mwanamke anayehusika ni cha kikatili kinachopaswa kukemewa sana,” alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mathias.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi ameomba wadau wenye taarifa yoyote inayohusiana na kichanga hicho waifikishe Polisi ili kufanikisha msako wa mtuhumiwa wa tukio hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment