Thursday, 26 June 2014

TAJIRI WA KICHINA APIGA MSOSI NA MASIKINI WA NEW YORK, AWAKAMATISHA BAADHI YAO DOLA 300 KILA MMOJA

Chinese millionaire Chen Guangbiao stands with men during a lunch he sponsored for hundreds of needy New Yorkers at Loeb Boathouse in New York's Central Park
Tajiri huyo(mwenye suti) akiwa na baadhi ya wakazi wa jiji la New York wasio na makazi rasmi
Baadhi yao wakipata msosi
TAJIRI wa kichina, Chen Guangbiao amewapigisha msosi zaidi ya 250 wa jiji la New York wasio na makazi na baada ya tukio hilo akawakamatisha baadhi yao Dola za Kimarekani 300 kila mmoja kama alivyoahidi kupitia mwaliko alioutoa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mamia ya masikini wa jiji hilo walijitokeza kwa wingi kuitikia wito wa tajiri huyo na kupata naye msoni katika tukio ambalo tajiri huyo aliiamba wimbo maarufu wa Michael Jackson na wanamuziki wengine mashuhuri duniani wa “We Are the World”.

Katika tukio hilo lililofanyika juzi katika mgahawa wa posh, tajiri huyo akijibatiza jina la mtu mwenye huruma zaidi dunia.

Hata hivyo wageni wake walipasuka kwa hasira baada ya kukosa mgao wa Dola 300  alizokuwa ameahidi.

Akizungumza na wanahabari wa kichina huku masikini hao wakiendelea kusambaziwa msosi, mmoja wao alisimama na kupiga kelele akimtaka tajiri huyo aache kudanganya watu, kwasababu wengi wao walikwenda katika hafla hiyo sio kwasababu walivutiwa na mpango wa kula chakula na tajiri lakini kwasababu waliahidiwa kuondoka na dola 300 kila mmoja.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment