Sunday, 1 June 2014

NCHEMBA KUISAMBARATISHA CHADEMA MJINI IRINGA HII LEO

Nchemba katika moja ya mikutano yake aliyofanya hivikaribuni mkoani Iringa, hapa ilikuwa Ifunda, jimbo 
KATIKA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa leo hii kitamtumia Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba kwa kile kilichoelezwa na wanaCCM wenyewe kukisambaratisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Tangu kuwasili kwa Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Hassan Mtenga ambaye pia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, chama hicho kimekuwa kikifanya shughuli mbalimbali za kisiasa zinazolenga kujiimarisha wakati kikijiandaa kwa uchaguzi huo.

Dawa kuu inayotafutwa na chama hicho ni ile itakayotibu kile kinachoelezwa kuwa na kwa uzembe na siasa zao za makundi zilizopelekea washindwe katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Katika mikutano yake mbalimbali na mahojiano ambayo amekuwa akiyafanya na wanahabari mara kwa mara, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa amekuwa akisisitiza kwamba siku za Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa (chadema) kuendelea kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo zina hesabika.

“Iwe iwavyo, mwaka 2015 ni lazima Mchungaji Msigwa ang’oke, atang’oka kwasababu ameshindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na anajua alipata nafasi hiyo kama zile ngekewa wanazopata wachache za kuokota pochi chooni,” alisema.

Katika mkutano wa leo utakaofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kuanzia saa nane, Nchemba atakuwa na viongozi wengine mbalimbali wa CCM wakiwemo mawaziri saba ambao hawajatajwa kwa majina yao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment