Monday, 2 June 2014

NANI KUNUSURU MAKUMBUSHO YA CHIFU MKWAWA YALIYOKO KALENGA MKOANI IRINGA?

Fuvu la Chifu Mk2wawa linavyoonekana hivisasa

Jengo ammbko fuvu hilo limehifadhiwa

Baadhi ya wanahabari waliotembelea hii wakifanya vitu vyao

Kulikuwa na maelezo marefu, mazuri na ya kusikitisha kutoka kwa muangalizi wa makumbusho, Zuberi Suleimani

Picha inayobeba kumbukumbu ya jemadari huyo

Pamoja na kupewa maelezo marefu ya historia nzuri ya Chifu wa wahehe, Chifu Mkwawa, makumbusho ya kingozi huyo shupavu yana mambo mengi ya kusikitisha.

Timu ya wanahabari kutoka Dar es Salaam na mjini Iringa imetembelea hii leo na kusikia kilio kutoka kwa wafanyakazi wa makumbusho hayo.

Huenda isifanane na makumbusho nyingine zilizoko nchini, lakini taarifa ambazo hazikuthibitishwa na wahusika wenyewe zinaonesha wafanyakazi wawali wa kituo hicho wanawajibika kama vibarua.

Kibarua ni mfanyakazi asiye na mkataba wa kudumu kazini anayelipwa ujira wake kwa makubaliano ya kazi fulani, kwa saa, siku au muda wowote atakaokubaliana na anayempa kazi.

Wafanyakazi wa makumbusho hiyo; bila kujali kama wameajiriwa au hawajaajiriwa wanafanya kazi zote zinazohusu kituo hicho kama vibarua.

Wanafanya kazi ya kusafisha mazingira ya makumbusho, kupokea wageni, kutoa maelezo ya makumbusho na nyingine nyingi zinazojitokeza, haikuelezwa kama ujira wanaopata unafanana na kile wanachofanya.

Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba katika makumbusho hiyo huwezi kupata huduma nyingine yoyote kama ya chakula, vinywaji, sehemu ya kupumzikia na burudani zingine kama ilivyo kwa makumbusho zingine nchini.

Wageni wanaotembelea makumbusho hiyo hujikuta wamechoshwa na mazingira yake kwani muda wote wawapo hapo husimama na hukosa huduma zingine zinazoweza kuwashawishi waendelee kuwepo.

Kiingilio cha Sh 20,000 kwa wageni kutoka nje kimeelezwa kuwa kikwazo kwani kimepunguza kwa kiasi nkikubwa wageni wan je wanaotembelea hapo.

Hata kiasi cha Sh 1,000 kinachotozwa kwa watanzania wanaotembelea hapo nacho kinapingwa kwa madai kwamba ni kikubwa na kuendelea kutozwa ni kuwakwamisha wananchi wasijue historia ya chifu huyo.

Makumbusho hayo hayana pia vipeperushi vya maelezo yake (bronchure) kama ilivyo kwa vivutio vinngine nchini.

Nani wa kukinusuru makumbusho haya ili malengo ya kuanzishwa kwake yasipote?

Reactions:

0 comments:

Post a Comment