Monday, 16 June 2014

MTIKILA AISHINDA TENA SERIKALI MAHAKAMANI


Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu yenye makao yake makuu jijini Arusha imetoa miezi sita kwa serikali ya Tanzania kuanza kutekeleza mchakato wa kuwepo kwa mgombea binafsi katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Jaji mkuu wa mahakama hiyo Mh. Sophia Akufo amesema kwa mujibu wa mkataba ulioridhiwa na nchi zote baada ya kutolewa kwa hukumu ni lazima utekelezaji wake ufanyike ndani ya muda uliopangwa utaratibu ambao bado haujafanyika baada ya hukumu ya kesi ya mgombea binafi kutolewa mwezi June mwaka 2013 .

Aidha Mh Akufo amefafanua kuwa pia serikali inawajibika kuweka hukumu maelekezo ya hukumu iliyotolewa ya haki ya kuwepo kwa mgombea binafi katika gazeti la serikali katika kipindi kisichozidi miezi tisa baada ya kutolewa utaratibu ambao pia bado haujatekelezwa

Tarehe 14 June mwaka 2013 mahakama hiyo ilitoa hukumu ya kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi iliyokuwa imewasilishwa mahakamani hapo na MTIKILA

Reactions:

0 comments:

Post a Comment