Thursday, 26 June 2014

LUIS SUAREZ AFUNGIWA MIEZI MINNE, KUKOSA MECHI TISA ZA KIMATAIFA NA LIGI KUU


Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez amafungiwa kucheza mpira katika ngazi zote kwa kipindi cha miezi minne baada ya kumng’ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.

Pamoja na maamuzi hayo, mshambuliaji huyo wa Liverpool ya Uingereza mwenye umri wa miaka 27 amefungiwa kucheza mechi tisa za kimataifa, uamuzi unaomtoa kwenye mashindano ya kombe la Dunia yanayoendelea nchini Brazil.

Kwa maamuzi hayo, Suarez atakosa mechi tisa za mwanzo za ligi kuu ya Uingereza au kokote kule atakakohamia.


Suarez alifanya tukio hilo Jumanne wakati timu za kundi D zikimenyana. Timu yake ya Uruguay imefuzu hatua ngumu ya 16 bora. 

Pamoja na maamuzi hayo ya FIFA, Uruguay wana nafasi ya kukata rufaa na wamepewa siku tatu za kufanya hivyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment