Thursday, 12 June 2014

LEO NI KATI YA BRAZIL NA CROATIA KATIKA UZINDUZI WA KOMBE LA DUNIA HUKO BRAZIL

Club rivals Neymar and Luka Modric square off in the 2014 World Cup opener.
Neymar wa Brazil na Modric wa Croatia katika action
Hatimaye ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil imetangazwa, huku wenyeji wa michuano hiyo, Brazil ikiikaribisha Croatia kwenye mechi ya kufungua dimba iliyopangwa kufanyika 12 Juni 2014.

 Kundi A linawakutanisha Brazil, Croatia, Mexico na Cameroon 'Simba Wasiofugika'.

Kundi B lina timu za Uhispania mabingwa watetezi, Uholanzi, Chile na Australia.

 Kundi C lina timu za Colombia, Ugiriki, Ivory Coast 'Tembo' na Japan. Inaelekea kuwa Kodivaa ' Tembo' ina nafasi nzuri ya kuingia hatua ya mtoano ya 16 bora.

Washindi wa zamani wa Kombe la Dunia, Uingereza, Italia, Uruguay pamoja na Coasta Rica wako kundi D.

Kundi E kuna timu za Uswisi, Ecuador, Ufaransa na Honduras. Ufaransa baada ya kuingia kwa mbinde kwenye fainali hizo, inatabiriwa na wadau wa soka kuingia hatua ya mtoano ka urahisi.

 Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo inacheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya nne, imepangiwa na nchi za Argentina, Bosnia Herzegovina na Nigeria "Tai wa Kijani' katika kundi F.

Kundi G, kuna timu za Ujerumani, Ureno, Marekani na wawakilishi wengine wa Afrika Ghana 'Black Stars'.

Na kundi H lina timu za Ubelgiji, Russia, Korea ya Kusini na wawakilishi wengine wa Afrika, Algeria 'Mbweha wa Jangwani'.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment