Wednesday, 4 June 2014

DEREVA NA TINGO WATUHUMIWA KUSHUHA MZIGO WA MITUMBA KATIKA ROLI NA KULICHOMA MOTO

RPC wa Iringa, Ramadhani Mungi
GARI aina ya Scania lenye namba T527 BPQ na tela namba T 976 BME limechomwa moto kwa makusudi baada ya kushusha na kuuza mzigo wa mitumba uliokuwemo ndani yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Ramadhani Mungi alisema watu sita wanachikiliwa na jeshi hilo wakihusishwa na tukio hilo.

Mungi amesema askari polisi wakiwa doria katika maeneo ya Mafinga, wilayani Mufindi Mkoani Iringa walikuta gari likiwa linaungua bila ya kuwepo kwa dereva wala tingo wake.

Baada ya uchunguzi walimbaini dereva wa gari hilo kuwa ni Elia Christiani mwenye umri wa miaka 26 na tingo wake Deusi Gembe Mwenye umri wa miaka 20 kuhusika na tukio hilo.

Alisema watuhumiwa hao waliwasha moto gari hilo baada ya kushusha kwa magendo  mzigo huo wa mitumba kwa mtu aliefahamika kwa jina la Agrey Mpinga na kukimbia.

Uchunguzi uliofanywa na Polisi unaonesha suala wizi huo una mtandao mkubwa unaowahusisha watu wengine watu, Masko Buhewa (53) ambaye ni mfanyabiashara katika kijiji cha Nyololo wilayani humo, Isack Buhewa (25) na Petro Kipera (26).

Katika katika lingine, jeshi hilo linawashikila watu wawili wakituhumiwa kujifanya wao ni askari Polisi.

Watu hao ni Bashili Nyakungu (20) aliyekutwa akiwa amevaa sare za jeshi la Polisi huku akiwatapeli watu kwamba anatoa nafasi kwa vijana wanaotaka kujiunga na jeshi hilo.

Akiwa na mtuhumiwa mwingine, Goodluck Mbeale (21) aliyejifanya bosi wa jeshi hilo, Nyakungu alikamatwa mkoani hapa wakati akichukua fedha kutoka kwa watu waliokuwa wakiamini angewasaidia kwa kuwapa nafasi hizo watoto wao.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment