Wednesday, 11 June 2014

CHADEMA MKOA WA IRINGA YAZIDI KUPATA PIGO

Selemani Kiponda akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga

Kisha akakabidhi bendara ya chama hicho iliyokuwa imetundikwa nyumbani kwake

baadaye akatawazwa kwa kupewa kadi ya CCM na Diwani wa Kata ya Ihimbo,Hezron Nganyagwa (CCM)

Na kisha akapewa bendera ya CCM ili akaipandishe nyumbani kwake
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Iringa kinazidi kubomoka pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi wake katika kukiimarisha.

Baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini, Emanuel Ngwalenje hivikaribuni kutimkia Chadema na wanachama wengine zaidi ya 100 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Iringa kwa nyakati tofauti walikikimbia chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katika tukio la juzi, Mwenyekiti Chadema kata ya Ihimbo , Selamini Kiponda amekiongezea kidonda chama hicho baada ya kujitoa na kuinga na CCM.

Kiponda alifikia uamuzi huo juzi kwa kile alichosema amekuwa kiongozi wa Chadema kwa  miaka minne na ameweza kushawishi wakazi wengi katika maeneo mbalimbali katika kata ya Ihimbo kujiunga na  chama hicho lakini hawajawahi kupata ushirikiano wowte kutoka uongozi wa mkoa na Taifa.

“Nilijiunga na Chadema mwaka 1993 wakati ndio kwanza upinzani umeingia nchini na nimekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya minne; hakuna ushirikiano wanachama wa Chadema huku vijiji tunahangaika kama kuku wa kienyeji tusiyejua baba wala mama yetu, nimechoshwa na sasa nimeamua kurudi CCM kwa kuwa ndio chama changu ambacho kwa kweli nilikuwapo tangu enzi za TANU,” alisema.

Alisema kurudi kwake CCM kumechagizwa zaidi na maendeleo yanayofanywa na diwani wa kata hiyo Hezron Nganyagwa pamoja na mbunge wa Jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla.

Akimpokea mwanachama huyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema Kiponda amefanya maamuzi sahihi na kwamba uamuzi wake unazidi kudhihirisha tofauti iliyopo baina ya vyama hivyo viwili.

Mtenga aliwaomba viongozi na wanachama wengine wa Chadema wilayani Kilolo kufuata nyayo za Kiponda kwa kuachana na Chadema inayohubiri vurugu badala ya maendeleo.

Naye diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa aliahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali Kiponda ili kwa pamoja waweze kutekeleza vyema Ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na Kilolo kwa ujumla.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment