Monday, 9 June 2014

CAMEROON WAGOMA KWENDA BRAZIL.


Kikosi cha Cameroon
Kikosi cha Cameroon

Zikiwa zimebaki siku chache fainaliza kombe la Dunia zianze nchini Brazil wawakirishi wa bara la Afrika Cameroon leo wameingia katika migogoro kati ya wachezaji na viongozi baada ya Wachezaji kugoma kupanda ndege hadi watakapo lipwa posho zao.
Mgomo huo wa wachezaji umetokea leo wakatika timu hiyo ikijiandaa kukwea pipa ili ikajiunge na wapinzani wao katika michuano hiyo inayo fanyikia Nchini Brazil kwa mwaka huu.
Cameroon ipo katika kundi A ambolo linaongozwa na wenyeji wafainali hizo Brazil, Maxico na Croatia.
Ndege ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi kwenda Brazil, wakati Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment