Thursday, 19 June 2014

BYE BYE SPAIN, YAAGA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA BAADA YA KULA KICHAPO CHA PILI MFULULIZO

bye bye Spain, yasubiri kukamilisha raundi ya kwanza ya makundi, yachapwa 2-0 na Chille
Mkosi umeendelea kuwaandamana mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la dunia, timu ya Taifa ya Spain baada ya usiku wa kuamkia leo kula kichapo cha mabao 2-0 na kuingia katika orodha ya timu za mwanzo zinazoaga mashindano hayo.

Baada ya Ufaransa bingwa wa 1998 kutolewa raundi ya kwanza 2002, Italy bingwa wa 2006 kutolewa kwenye makundi 2010, historia hiyo imejirudia tena baada ya bingwa wa 2010, timu ya Taifa ya Spain maarufu kama La Roja kuaga mashindano hayo.

Wakicheza mechi yao ya pili dhidi ya Chile, La Roja wamevuliwa ubingwa kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chile.


Alikuwa Eduardo Vargas kwenye dakika ya 20 aliifungia Chile goli la kuongoza, lakini mchezaji CH. Aranguiz akafunga kazi kwa kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Spain.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment