Thursday, 26 June 2014

BOATENG NA MUNTARI WAONDOLEWA KIKOSI CHA GHANA

Kevin-Prince Boateng and Sulley Muntari

Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wamefukuzwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kinachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuonesha utovu wa nidhamu.

Taarifa ya Chama cha Soka cha Ghana imesema wachezaji hao “wamesimamishwa kwa kipindi kisichojulikana.”

Tarifa hiyo imeongeza wakati Boateng anahusishwa na matumizi ya lugha mbaya kwa kocha Kwesi Appiah, Muntari alifanya shambulizi kwa mmoja wa wajumbe wa kamati tendaji ya chama hicho.

Wachezaji hao wameondolewa katika kikosi hicho ikiwa ni masaa machache kabla ya leo kuvaana na Ureno. Ghana wanaweza kuingia hatua ya 16 bora kama watashinda kwa magoli mengi mechi na kama Marekani ambayo wako kundi moja watafungwa na Ujerumani.

Ghana inaingia katika mechi hiyo ya mwisho ya makundi ikiwa na pointi moja sawa na Ureno, huku Ujerumani ikiwa na pointi sita huku Marekeni ikiwa na pointi nne.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment