Monday, 23 June 2014

AJALI MBAYA YATOKEA LUGEMBA MAFINGA, MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU IRINGA ANUSURIKA, DERVA AFARIKI PAPO HAPO


baada ya ajali hiyo, 
Inavyoonekana kwa nyuma
hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo
Scania lililogongwa kwa nyuma
Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia
AJALI mbaya iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368 CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa Mafinga.

Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya roli hilo lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es Salaam, akiwa katika mwendo mkali.

Mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 usiku. Na baada ya ajali hiyo wasamalia wema waliukumbiza mwili wa marehemu na majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa za awali zinaonesha dereva wa gari hilo alikuwa amelewa wakati akiendesha gari hilo.
  

Reactions:

1 comments:

  1. Poleni sana madereva muwe makni

    ReplyDelete