Sunday, 25 May 2014

PROFESA MSOLLA ATAKA SOKA KILOLO ITOE WACHEZAJI WENYE HADHI YA DROGBA NA MESSI


Profesa Msolla akitoa msaada wa seti ya jezi wa kapteni wa timu ya wavulana ya kijiji cha Kidabaga
Hapa akitoa mpira wa kwa timu ya netball

MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla ameendelea kuhamasisha michezo katika jimbo lake hilo kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za vijana na wanawake za vijiji mbalimbali.

Katika ziara yake aliyofanya hivi karibuni katika vijiji vya Lulanzi, Kilolo, Kitowo,  Lusinga, Ndengisivili na Kidabaga, Prpfesa Msolla alitoa jezi, mipira na vifaa vingine vya michezo kwa timu za soka na mpira wa pete zinazoundwa na wavulana na wasichana katika vijiji hivyo.

“Michezo hujenga afya, michezo ni uhai; inatuepusha na tamaa zingine za dunia na hatari ya ulevi wa kupindukia na ngono zembe, lakini michezo ni ajira ya uhakika,” alisema.

Alisema michezo hasa wa soka umekuwa ukiwatajirisha vijana duniani kote na akataka vijana wa Kilolo kuitumia fursa hiyo kujenga afya zao huku wakijua kwamba ni ajira inayolipa kuliko ajira nyingi duniani.

“Wako wachezaji wanalipwa zaidi ya Sh Milioni 300 kwa wiki; mnawasikia akina Messi, Ronaldo na kwa Afrika tunao wengi tu kama akina Drogba, Yaya Tour, Etoo na wengine wengi,” alisema.

Alisema vijana wa Kilolo na wengine kutokana maeneo mbalimbali nchini wanaweza kufikia viwango vya wachezaji hao kama wataweka dhamira.

“Hata timu zetu kubwa za Yanga na Simba zinalipa vizuri, mnajua kwasababu mnasikia wachezaji wanavyosalijiwa na mikataba yao minono wanayopata,” alisema.

Akiwa katika kijiji cha Kidabaga, Profesa Msolla alipewa ombi la kusaidia ujenzi wa michezo na akaahidi kwa kupitia mfuko wa jimbo kuangalia uwezekano wa kufanya hivyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment