Sunday, 25 May 2014

NGUMI ZATAKA KUPIGWA MOCHWARI MWILI WA MAREHEMU WASUBIRISHWA KWA DAKIKA CHACHE SOMA HABARI HII KWA MAELEZO ZAIDI

Hili ni tukio la aina yake lililotokea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa nje  ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mutually).
Ambapo maiti ya aliyekua msanii maarufu wa filamu mkoani Iringa Marehemu Abisai Mdessa(Kisandaki)-(28) aliyefariki kwa ajali ya bodaboda iliyotokea maeneo ya ndiuk mkoani iringa  ambapo marehemu alipata majeraha mmengi kichwani  hali iliyopelekea kifo chake mnamo Tarehe 23/05/2014.
Shughuli ya mazishi zilifanyika nyumbani kwao Tanangozi Tarehe 24/05/2014 ambapo mamia ya madereva wa bodaboda na wakazi wa maeneo mbalimbali nan nje ya mmkoa wa Iringa walihudhuria mazishi hayo. Lakini katika hali iliyoshangaza wengi ni pale Malumbano ya kisiasa yaliyoanza  baina ya Mwenyekiti wa chama cha bodaboda mkoa wa Iringa Bw Bw Joseph Mwambobe, na Mkereketwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Bw Chagu Michael, bajaji iliyoteuliwa kubeba mwili wa marehemu ilifungwa bendera ya CHADEMA ndipo vuta nikuvute ilipoanza kati ya makundi hayo mawili.
 Bw Bw Joseph Mwambobe, Mwenyekiti wa chama cha bodaboda mkoa wa Iringa
Bw Chagu Michael-Mwanaharakati wa CHADEMA

Marehemu Abisai Mdesa(Kisandaki) Enzi za Uhai wake

Bw. Luckson Luswema Afisa Uhusiano Iringa MuviMaelfu ya Bodaboda Wakiwa Katika Msafara Kuelekea Tanangozi

Wadau wa Sanaa Panoja na Madereva wa Bodaboda Wakiinua Mwili wa Marehemu Ili kutoa Heshima Zao za Mwisho

Picha Iliyoinuliwa Ni Marehemu Abisai Enzi za Uhai
“Huu ni msiba unaowahusu Wanabodaboda mkoa wa Iringa na si wa wanachadema peke yao hivyo hatuhitaji itikadi za kisiasa” Alisema Mwenyekiti huyo wa Wanabodaboda
Kwa upande wake Mwanachadema huyo alidai sababu za wanachadema kutaka kupeperusha bendera yao ni Kwa sababu marehemu huyo alikua ni mfuasi wa CHADEMA.
Hata hivyo mtandao huu (BONGOLEAKS)  ulibaini kwamba wanaCHADEMA hawakuwa na sababu ya kutaka kupeperusha bendera yao ikiwa hawakuto usafiri wa kubeba mwili wa marehemu wao kama wanachadema bali usafiri huo ulitolewa na wanabodaboda wote bila kujali itikadi za Kisiasa.
Kwa Heri Abisai Mdesa
Msiba wa Marehemu Abisai Mdesa unawekwa katika rekodi za watu waliowahi kuzikwa na watu wengi Zaidi Mkoani Iringa Hii ni kutokana na Pikipiki (Bodaboda) Zaidi ya 500 kushiriki katika mazishi hayo.
Marehemu Abisai Mdesa(KISANDAKI) Licha ya kuwa Dereva wa Bodaboda Alikuwa na Msanii tegemeo katika kikundi cha MUNDU SANAA GROUP(POLISI JAMII) Na aliwahi kuigiza filamu kama Vile STRESS,YOSHUA PAMOJA NA POLISI JAMII zilizoandaliwa na kikundi maarufu cha Sanaa mkoani Iringa MUNDU SANAA GROUP Pia alishiriki muvi itakayokujia hivi karibuni iitwayo “I MUST REVENGE” ambapo marehemu aliigiza kama Teja au muathirika wa madawa ya kulevya inayoandaliwa na “THE NEXT STEP PRODUCTIONS LTD”.

Bwana alito na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe!
Inna lillah wainna illah raajuunii(Sote ni wa Mungu)


Reactions:

0 comments:

Post a Comment