Friday, 30 May 2014

MASIKINI HAPPY MAGESE, ASIMULIA KILIO CHAKE CHA MIAKA MINGI

Happy Magese

UGONJWA wa Endometriosis umefanya Miss Tanzania 2001 ambaye kwasasa ni mwanamitindo wa kimataifa, Happines Magese kushindwa kubeba ujauzito

Kutokana na kukumbwa na tatizo hilo, Magese kupitia kampuni yake ya Millen Magese ameanzisha kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zai wanaposumbuliwa na ugonjwa huo.

Amesema wanawake na wasichana wengi hapa nchini wanalo tatizo hilo lakini kwa kuwa hawajui kama ni tatizo linahitaji utafiti mapema wamekuwa wakikosa suluhisho.

“Huu ni ugonjwa ambao umenitesa kwa muda mrefu na umeniathiri, leo siwezi kuolewa kwasababu sina uwezo wa kubeba mimba, ni mwanamme gani atakubali kukaa na mwanamke asiyezaa,” alisema alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam juzi.

Kwa kuanzia alisema jumapili ya wiki hii watatoa mafunzo kwenye fuko za Coco kwa kuelimisha watu athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo.

Alihimiza wadau mbalimbali kuwainga mkono huku akiahidi kujenga hospitali ya wanawake mjini Dodoma kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo ili kuwaokoa wanawake wengi kwa gharama nafuu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment