Tuesday, 6 May 2014

DHAHABU NJE NJE WILAYANI MUFINDI, WACHIMBAJI WAHOFIA USALAMA WAO

bonge la dhahabu
MACHIMBO mapya ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Ihanzutwa wilayani Mufindi mkoani Iringa yameelezwa kukusanya wachimbaji zaidi ya 1000.

“Dhahabu inatoka kweli kweli, wachimbaji wako wengi katika machimbo haya na kiukweli mambo sio mabaya,” alisema mchimbaji ambaye hakuta kutajwa jina.

Alisema tatizo pekee liliko katika machimbo hayo yaliyopo takribani kilimita 60 kutoka mjini Mafinga ni ulinzi na usalama.

“Kuna wageni wengi, baadhi yao wanaonekana hawako katika machimbo hayo kwa nia njema, tuna mashaka nao,  kimsingi wana tisha na hali haiku shwari,” alisema.

Alisema zipo taarifa za baadhi yao kuwa na silaha kali za moto na haileweki kwanini wanazimiliki wazi wazi katika eneo hilo.

Alisema taarifa za kuwepo kwa watu hao zimetolewa kwa uongozi wa jeshi la Polisi lililoonesha kuzifanyia kazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi hakuweza kupatikana kuzungumzia kwa kina hali ilivyo katika machimbo hayo.


Mtandao huu utakujuza taarifa itakazozipata kuhusiana na hali ya usalama na hatua zilizochukuliwa na jeshi la Polisi wakati wowote kuanzia sasa. Endelea kupitia mtandao huu nkwa habari mbalimbali za mkoa wa Iringa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment