Friday, 9 May 2014

DEREVA WA HALMASHAURI IRAMBA AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI

DSC0017911

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
DEREVA wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Juma Juma (52) amefariki dunia wakati akifanya mapenzi na mwanamke mhudumu wa baa kwenye nyumba ya kulala wageni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea mei tatu mwaka huu saa nane za usiku chumba no.S.2 nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New Kiomboi mjini.

Amesema siku ya tukio,dereva Juma saa sita za usiku alimwaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hatachelewa kurudi nyumba kwa kwa hiyo alifunga mlango wa mbele ya nyumba.

Amesema kuwa saa mbili baadaye Juma alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba hiyo la kulala wageni iliyoko umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwake.

“Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo alitwaye Agness Mayo (32) anayesadikika kuwa na uhusinao wa kimapenzi na Juma.”,amesema. 

Kamwela amesema mhudumu huyo wa baa mpenzi wa Juma,alitoweka mei nne mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.Hata hivyo,ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wa baa.

Kamanda huyo amesema kuwa toka siku hiyo ya mei tatu chumba alicholala Juma hakifunguliwa hadi mei tano mwaka huu na ndipo mwili wa dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika vibaya.

“Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili endapo atabainika kuhusika na tukio hilo”,amesema Kamanda Kamwela

Reactions:

0 comments:

Post a Comment