Friday, 25 April 2014

MPANGO WA MANISPAA YA IRINGA KUVUNJA KILABU CHA MIVINJENI UPO PALE PALE


Eneo la kilabu cha Mivinjeni linalotafutiwa mwekezaji, majengo yanayoonekana ndio kilabu chenyewe


Eneo la Gangilonga Zone II
MIPANGO ya halmashauri ya manispaa ya Iringa kuvunja kilabu cha pombe za kienyeji cha Mivinjeni iko pale pale ili kupisha uwekezaji mkubwa.

Hata hivyo jitihada za manispaa hiyo kutafuta mwekezaji mwenye sifa zilizotajwa zinaelekea kugonga mwamba kwa mwaka tatu sasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo, Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gerva s Ndaki amesema eneo hilo lililopo jirani na Chuo cha Ufundu Stadi cha VETA Iringa lina ukuba wa mita za mraba 6,643.

Mwekezaji anayetakiwa kupewa eneo hilo ameelezwa na na manispaa hiyo kwamba ni lazima awe tayari kujenga kumbi kwa ajili ya muziki, sherehe, bar, hoteli na mazoezi, maduka makubwa, bwawa la kuogoelea na sehemu ya maegesho ya magari.

Eneo lingine linalotafutiwa mwekezaji lipo Gangilonga Zone II lenye ukubwa wa mita za mraba 4,655 ambalo halmashauri hiyo linataka liwekezwe kwa kujenga kumbi za mikutano za ukubwa mbalimbali, hoteli, na maegesho ya magari.

Eeneo hilo lipo nyuma ya Kanisa la Anglikana karibu kabisa mahakama kuu kanda ya Iringa na ofisi ya mkuu wa wilaya.

Pamoja na wadau wa maendeleo ya manispaa ya Iringa kuitaka manispaa hiyo kuyatangaza upya maeneo hayo, mtandao huu unatoa wito kwa wawekezaji wenye uwezo kuchangamkia fursa hizo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment