Tuesday, 22 April 2014

DAVID MOYES ATIMULIWA RASMI MAN UNITED, RYAN GIGGS APEWA JUKUMU LA MUDA


Kibarua cha David Moyes United chafika mwisho
 Manchester United imethibitisha Jumanne ya jana kwamba meneja wake David Moyoes amapigwa chini.

Moyes alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sir Alex Ferguson, majira ya joto mwaka jana akipewa mkataba wa miaka sita.

Taarifa iliyotolewa kwenye Mtandao wa klabu hiyo  imesema: “Manchester United inatangaza kwamba David Moyoes ameondolewa klabuni.

 “Klabu inapenda kuweka rekodi sawasawa, ikimshukuru kwa kazi ngumu aliyofanya, uungwana na utu alioonesha kwenye klabu.”

Ryan Giggs, aliyefanya kazi kama kocha mchezaji chini ya Moyoes msimu huu, atachukua majukumu ya muda ya kuinoa klabu.

Mmoja wa makocha wanaotajwa kurithi mikoba ya Moyes ni pamoja na Juergen Klopp, hata hivyo Borussia Dortmund  imekanusha uvumi huo ikisema hakuna nmana yoyote kwa kocha huyo kujiunga na United.

United imekanusha pia kufanya mazungumzo na Louis van Gal, anayetarajia kumaliza mkataba wa kuinoa timu ya Taifa ya Uholanzi baada ya Fainali za Kombe la Dunia.

Hata hivyo gazeti la Uholanzi la De Telegraaf limethibitisha Jumanne ya jana kwamba kocha huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich alikuwa akielekea Ureno kwa mazungumzo na Mwenyekiti Mwenza wa United, Joel Glazer.

Mlinzi wa zamani wa United, Laurent Blanc, ambaye kwasasa ni meneja wa Paris Saint-Germain, anatajwatajwa kupewa kibarua hicho pamoja na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone, pamoja na kwamba mu Argenitina huyo hazungumzi kingereza.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment