Wednesday, 9 April 2014

CHELSEA HIYOOOOO NUSU FAINALI UEFA

Demba Ba scores the dramatic 87th-minute goal which edged Chelsea past PSG.
Demba Ba akimalizia vitu vilivyoifanya Chelsea iingie nusu faini ya mabingwa wa Ulaya baada ya kuilaza PSG kwa mabao 2-0

NDOTO za Chelsea na Jose Mourinho kunyakua kwa mara nyingine kombe la Mabingwa Ulaya  (UEFA Champion) zinaelekea kutumia baada ya kufanikiwa kubadili matokeo kwa kulazimisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Paris St Germain na kufuzu nusu fainali ya kombe hilo.

Mourinho alikimbia umbali mrefu kuungana na wachezaji wake kushangilia goli la ushindi lililofungwa katika dakika ya 78 ya mchezo huo na mchezaji wa akiba Demba Ba.

Chelsea ilifungwa bao 3-1 katika mchezo wake wa kwanza ikiwa nyumbani kwa PSG, lakini rekodi yake ya kutofungwa katika uwanja wake wa nyumbani tangu Setptemba mwaka jana, iliiwezesha kujipatia ushindi huo.

Mashabiki wa Chelsea waliitia moyo timu hiyo iliyojipatia goli lake la kwanza katika dakika ya 32 kupitia kiungo wake Andre Schurrle .

Reactions:

0 comments:

Post a Comment