Wednesday, 19 March 2014

WAWILI WASHIKILIWA KWA MAUAJI NJOMBE
RPC Fulgance Ngonyani
Jeshi la Polisi mkoani njombe linawashikilia  Matrida Chaula na Dominicus  Luoga wakihusishwa na matukio wawili tofauti ya Mauaji.

Taarifa ya jeshi hilo imesema mtuhumiwa Matrida Chaula ambaye ni mkazi wa wilaya ya Mekete anahojiwa na Polisi akihusishwa na tukio la mauji ya Frank Sanga.

Sanga alikutwa akiwa amefariki chumbani mwa mtuhumiwa huyo baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni kisu; alichomwa sehemu ya kifuani na Yohana Sanga anayedaiwa kutoroka baada ya kufanya tukio hilo.

Polisi pia wanamshikilia Dominicus  Luoga, mkazi wa Ibumi wilayani Ludewa kwa mahojiano ya mauaji ya Jane Luoga aliyafariki baada ya kuchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa kisu shingoni mwake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Fulgance Ngonyani alisema matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti katika wilaya hizo Machi 17, mwaka huu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment