Wednesday, 12 March 2014

WANANCHI MPANDA WAASWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

???????????????????????????????
Add caption
Na Kibada Kibada –Katavi
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wamepewa changamoto ya kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi  mazingira ,  kwani kuharibu mazingira  kunachangia ukame na kukosekana kwa maji ambayo  ni uhai wa viumbe na tegemeo la maisha ya wanadamu na wanyama.

Changamoto hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Kibiriti Yasini wakati akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Milala,  Kata ya Kabungu kwenye  maandalizi ya wiki ya maji inayotarajiwa kufanyika machi 22 mwaka huu.

Kibiriti amewataka kutoa ushirikiano wa karibu  kuhakikisha wanatimiza wajibu wake katika kulinda, kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Katika hotuba yake hiyo alisisitiza wananchi watoe ushirikianao wa dhati  kutunza vyanzo vya maji na kuilinda miradi ya maji iliyopo katika kijiji hicho na kuiona kuwa ni mali yao  na itawasaidia kwa manufaa ya wote. 

Akizungumzia  maandalizi ya wiki ya  maji kila mwaka  alisema huambatana na utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira, na uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala ambapo kwa kutambua  umuhimu serikali imefanya juhudi za kuhakikisha inawaondolea wananchi wake kero ya upatikana wa maji na kuwasogezea karibu wananchi maji.

Alieleza kuwa Katika kijiji cha milala vituo kumi vya kuchota maji vimejengwa na wananchi watapata maji  na  kuondokana na kero iliyokuwa ikiwakabili wakazi hao.

Alisema  Halmashauri yake kwa kushirikiana na Serikali kuu kwa kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa Big Results Now  (BRN) ndio siri ya mafanikio haya.

Hata hivyo amemwagiza Kaimu Mhandisi wa maji katika Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wa kijiji cha Milala wanaondokana na kero ya ukosekanaji wa maji.

Kwa upande wa upatikanaji wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda  ni wastani wa asilimia 48 tu ambapo hali hiyo ni kiasi kidogo, huku lengo ni kuhakikisha asilimia hiyo inaongezeka angalau kila kijiji kiwe na maji ya uhakika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment