Thursday, 6 March 2014

WAJASIRIAMALI 200 IRINGA WAPIGWA MSASA WA BIASHARA NA MASOKONaibu Meya, Gervas Ndaki akifungua mafunzo hayo
wajasiriamali

ZAIDI ya wajasiriamali 200 wa mjini Iringa wamepigwa msasa wa elimu ya biashara na masoko ili waboreshe shughuli zao za kiuchumi.

Mafunzo hayo yalitolewa na kampuni ya Vannedrick ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.

Mratibu wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Maendeleo mjini hapa, Anzawe Chaula alisema kabla ya mafunzo hayo, utafiti walioufanya unaonesha kuwepo kwa changamoto nyingi zinazokwamisha ukuaji wa biashara za wajasiriamali wadogo.

“Biashara nyingi zinazoanzishwa na wajasiriamali hao hazina dalili ya kukua kwasabbabu , waanzishi wake hawana maarifa ya biashara na masoko,” alisema.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia wajasiriamali kutambua fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa na kuzitumia ipasavyo ili wajikomboe kiuchumi.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku moja, Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa, Gervas Ndaki alisema ni muhimu kwa wajasiriamali na kama watayatumia kikamilifu yatazidisha matumizi ya fursa walizonazo katika kukuza biashara zao.

“Yanaweza kuwasaidieni kulete mabadiliko makubwa; na kwa upande wa wanawake yanaondoa ile dhana ya wanawake hawawezi,” alisema.

Ndaki aliwataka wajasiriamali hao kuacha kufanya shughuli zao kwa mazoea kwa kuhakikisha maarifa waliyopata yanawaletea mafanikio makubwa.

Alisema itapendeza kama wahusika watakaporudi tena watakuta kuna mabadiliko makubwa miongoni mwa wajasiriamali hao.

Alizitaka taasisi za kifedha hasa benki kupunguza masharti ya mikopo kwa wajasiriamali huku akiiomba serikali kutoa hamasa kwa asasi za kifedha kushirikiana na wajasiriamali wadogo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment