Tuesday, 25 March 2014

UJENZI WA JENGO LA HANS POPE WA SIMBA UNAOENDELEA MJINI IRINGA WALETA KERO KWA MAJIRANI

Hili ni jengo la Hans Pope na familia yake linalojengwa mjini Iringa, Karibu na hotel ya MR; jengo hili litakapokamilika ndilo litakalokuwa refu kuliko yote mjini Iringa; Ni hoteli itakayokuwa na ghorofa tisa, ujenzi wake unaendelea kwa usimamizi wa makandarasi toka China

Hapa ndipo penye kero inayolalamikiwa, kama inavyoonekana pichani, mabati ya uzio wa jengo linalojengwa yanazidi kuangukia nyumba ya pili na kwa muda mrefu sasa hakuna jitihada zinazofanywa za kuondoa hali hiyo. Wanaolalamika wanasema wanakosa fursa ya kufanya mambo yao mengi katika uchochoro huo ikiwa ni pamoja na kuutumia kama njia ya mkato

Reactions:

0 comments:

Post a Comment