Sunday, 9 March 2014

TIGO YASOGEZA HUDUMA ZAKE MKOA MPYA WA NJOMBE

DC wa Njomba, Sarah Dumba akizindua kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni ya simu ya Tigo mjini Njombe, pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Nyanda za Juu Kusini,, Jackson Kiwaga

Hapa alipongeza kampuni hiyo kwa jitihada zake za kusogeza huduma kwa wateja wake

Kiswaga akiwapongeza wachapa kazi wake
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Tigo imeanzisha kituo cha huduma kwa wateja wake katika mkoa mpya wa Njombe.

Kituo hicho kilifunguliwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba aliyeondoka na zawadi ya simu mpya ya mkononi aina ya Huawei.

Akizundua kituo hicho, Dumba alisema kitaharakisha huduma kwa wateja wa mtandao huo pendwa wa vijana.

“Niipongeze kampuni ya Tigo kwa kuwa ya kwanza kuleta huduma hii mkoani hapa; nina hakika hii itawaongezea imani kwa wateja wenu na kuchochea wateja wapya kujiunga nanyi,” alisema.

Alisema kuanzishwa kwa kituo hicho kutaongeza ajira miongoni mwa wakazi wa mkoa wa Njombe watakaotaka kuwa mawakala wa kuuza vocha, simu za tigo na huduma ya Tigo pesa.

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga alisema kituo hicho kimeanzishwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.

“Huduma za kaampuni yetu zinakuwa kwa kasi kubwa, tunazidi kupanuka, sasa tumefika katika moa huu mpya kwa mataarajio ya kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wetu,” alisema.

Alizitaaja huduma zitakazokuwa zikitolewa katika kituo hicho kuwa ni pamoja na huduma za mtandao wa tigo kwa ujumla, uuzaji na urejeshaji wa namba za simu, uuzaji wa simu za aina mbalimbali na utoaji wa huduma za uwakala.

Akizungumzia kukua kwa huduma ya Tigo Pesa, Kiswaga alisema kampuni hiyo ina mawakala zaidi ya 20,000 nchini na kwamba kufunguliwa kwa kituo hicho kunalenga kusogeza huduma hiyo katika wilaya za mkoa huo.

Akizungumzia changamoto za ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini alisema gharama kubwa ya usambazaji huduma hiyo unachelewesha huduma hiyo kufika kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini.

“Uwekezaji kwenye mitandao hii ni gharama kubwa, kwenda kila kijiji inakuwa shida kwasababu marejesho yake yanachukua muda mrefu,” alisema.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Kiswaga aliipongeza serikali kwa kuanzisha mfuko maalum wa uwekezaji vijijini utakaoziwezesha kampeni za simu kukopa fedha huko kwa ajili ya kuwekeza vijijini. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment