Tuesday, 18 March 2014

SHIRIKA LA TRACED LAZUNGUMZIA USAWA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Resource and Assessment Centre for Children with Disabilities (Traced) lililoundwa kwa hiari ya wazazi wa watoto wenye ulemavu kwa kushirikiana  na wataalamu wa fani ya elimu, afya, maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii wilayani mufindi  limewataka  wazazi kuwatoa watoto wenye ulemavu ili wapate haki kama wanazopata wasio na ulemavu.

Mratibu wa shirika hilo Stevin Mkandawile amesema shirika hilo kwasasa limejipanga kuhakikisha watoto wenye ulemavu, yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi wanapata fursa ya usawa katika jamii.

Amesema mlemavu anapochangamana na wasio na ulemavu anapata faraja na kuongeza thamani ya utu wake tofauti na akiwa anafungiwa ndani.

Mkandawile ameitaka jamii kuonyesha ushirikiano kwa shirika lao linaloendeshwa kwa hisani ya taasisi mbaalimbali.


Shirika hilo linahudumia watoto 170 waliopatikana katika kata 7, nne zikiwa za Mafinga mjini na tatu za nje ya mji wa mafinga.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment