Sunday, 9 March 2014

CHADEMA YAANZA KIVINGINE WIKI YA LALASALAMA UCHAGUZI MDOGO KALENGA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kimeanza wiki ya lalasama ya uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa, kikifanya kampeni zake kwa kutumia helkopta.

Wakati Chadema na mgombea wao Grace Tendega wakitumia helkopta, Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wake kinaendelea na kampeni zake za ardhini kwa kutumia magari.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu aliponda kampeni hizo akisema ni matumizi mabaya ya fedha za ruzuku na wadau wanaokichangia chama hicho kitakachoshindwa vibaya katika uchaguzi huo.

“Ndio mpaka sasa tumeshajihakikishia ushindi kwa asilimia kubwa; na hili litakuwa fundisho kubwa na nadhani baada ya hapo badala ya kutumia mamilioni kukodi helkopta kwa ajili ya kempeni zake, kitaanza kujenga ofisi na kulipa viongozi wake wa ngazi za chini,” alisema.

Alisema Chadema wanatumia helkopta kwenye shughuli zao za kisiasa kwasababu hawataki kujua na hatimaye kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo.

Jana helkopta ya Chadema ilizua tafrani katika maeneo ya mji wa Iringa baada ya kudondosha vipeperushi vyao mgombea wao Grace Tendega vilivyodhaniwa noti za elfu kumi kumi na wananchi wa Iringa.

Vipeperushi hivyo vilidodoshwa katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa na zilipo ofisi za CCM Mkoa wa Iringa.

Wakati ikidodosha vipeperushi hivyo helkopata hiyo iliyokuja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa ilikuwa ikipita juu kidogo ya majengo ya mji wa Iringa kabla ya kuelekea katika vijiji vya jimbo la Kalenga.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment