Monday, 10 February 2014

WAFANYABIASHARA IRINGA WAGOMEA MASHINE ZA EFD, WAFUNGA MADUKA, HATMA YA HUDUMA KUJULIKANA LEO JIONI


Mtaa wa makorongoni

Mtaa wa Miyomboni

Miyomboni

Stendi Kuu ya mabasi ya Iringa
Mtaa wa Mshine tatu

Mtaa wa Soko Kuu
Mtaa wa Uhindini
Stendi ya Mabasi Miyomboni

MGOMO uliofanywa kila kona ya mji wa Iringa na wafanyabiashara wa jumla na rejareja wanaopinga matumizi ya mashine za kodi za kielektroniki (EFD) umeathiri huduma za jamii mjini hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma amewataka kurejea kwenye biashara ili kunusuru hali hiyo na mapato ya biashara zao.

“Wengine wana mikopo; kwa faida yao, ya jamii na kwa maendeleo ya mkoa wa Iringa naomba warudi kwenye biashara wakati serikali ikichukua kilio chao na kukifanyia kazi,” alisema.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Ishengoma

Taarifa za wafanyabishara hao ya kufunga maduka yao mpaka pale serikali itakapositisha matumizi ya mashine hizo, ilianza kuenea juzi kwa kupitia mitandao ya simu na taarifa kutoka kwa kikundi kinachoendesha kampeni hiyo.

Mapema leo asubuhi wamiliki wa maduka makubwa, ya kati na madogo yaliyoko katikati ya mji wa Iringa na mitaa yake waliitikia mwito huo na kufanya wananchi wakose huduma walizokuwa wanahitaji.

Biashara pekee zilizokuwa zikiendelea kwa jana ni zile za vyakula katika masoko mbalimbali ya mjini Iringa.

Maduka ya nguo, vyakula, pombe, bar na hata baadhi ya kunyolea nywele yalifungwa na kufanya maeneo yamji wa Iringa yenye msongamano mkubwa kukaukiwa watu.

Hadi tunakwenda mitambani wafanyabiashara hao waliendelea kujikusanya ili kwa pamoja wafikie makubaliano yatakayotoa muongozo wa mgomo huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Iringa, Lucas Mwakabungu alisema wamepanga kukutana na wafanyabiashara hao saa tisa mchana wa leo ili kuwashauri wasiendelee na mgomo.

“Tunachukua kero yao na tunawaahidi tutakaa meza ya pamoja na serikali ili tufikie muafaka; mfanyabishara nayajua umuhimu wa mzunguko wa fedha yake hatakiwa kupoteza mapato kwa migomo kama hii,” alisema.

Mmoja wa wafanyabishara walioitikia mgomo huo, Boniface Bukuku alisema yeye ni mmoja wa wafanyabishara wa vitu vya urembo anayetakiwa kununua mashine hizo.
 
Mmoja wa wafanyabishara aliyegoma, Boniface Bukuku
“Alisema kwa mwaka amekadiriwa kulipa kodi ya Sh 574,000 kwa mwaka akiweka na mashine hiyo atalazimika kulipa fedha nyingi zaidi TRA,” alisema.

Akitoa mfano alisema kama mapato yake kwa mwezi ni Sh Milioni 2, atatakiwa kulipa wastani wa Sh200,000 kila mwezi kama kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Kwahiyo kwa mwaka nitatakiwa kulipa Sh Milioni 2.4 pamoja na makadiro ya kodi ya Sh 574,000, jumla natakiwa kulipa kiasi kinachokaribia Sh Milioni 3,” alisema.

Alisema kiasi hicho cha kodi ni nje ya kodi ya pango, mishahara ya wafanyakazi na huduma zingine za uendeshaji.

“Mwisho wa mwaka unawezajikuta kwa biashara ya mtaji wa Sh Milioni tatu, unatumia zaidi ya Sh Milioni sita kwa kodi ya serikali, kodi ya pango na mishahara na gharama zingine za uendeshaji kama umeme,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment