Tuesday, 11 February 2014

MSITU WA SAOHILL WAKABIDHIWA VITENDA KAZI VYA BILIONI 2.3


Orodha ya vitendea kazi kama sehemu yake inavyoonekana

DC Mufindi, Evarista Kalalu akikabidhi kwa Shio Godfrey wa Tarafa I ya msitu huo

Akikabidhi kwa Mohamed Borry mtumishi wa tarafa ya II

Akikabidhi kwa furaha kwa Ronald Machage wa Tarafa ya III ya msitu huo

Akikabidhi kwa William Dafa wa tarafa ya IV ya msitu huo

Akikabidhi Kijiko kwa Meneja Msaidizi anayeshughulikia Mipango na Matumizi, Mandalo Salum

Najua kuendesha bwana! hapa akijaribu kuondesha greda


Katika picha ya pamoja na viongozi wa msitu huo

Katika picha ya pamoja na watumishi wengine wa msitu huo

ZAIDI ya Sh Bilioni 2.3 zimetumiwa na Shamba la Miti la Sao Hill lililopo wilayani Mufindi mkoani Iringa kununua vitendea kazi mbalimbali.

Vitenda kazi hivyo ni pamoja na magari ya aina mbalimbali nane, pikipiki 25, greda moja na kijiko cha kusembua barabara.

Hafla ya makabidhiano ilifanywa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu kwa watumishi watakaovitumia vitendea kazi hivyo.

“Nakumbuka ilikuwa mwaka 2009, uongozi wa shamba hili ulipoelezea kero ya ukosefu wa vitendea kazi na kuiomba serikali iwaruhusu kununua kwa kupitia mapato yake yenyewe,” alisema.

Alisema matarajio ya serikali ni kuona vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuboresha malengo ya shamba hilo.

“Msitumie kwa shughuli zenu binafsi, tumieni kuboresha shughuli za shamba hili; tunataka kuona tofauti ya maendeleo ya shamba na mapato yake baada ya kuvipata,” alisema.

Awali, Meneja Msaidizi anayeshughulikia uendelezaji wa shamba hilo, Shadrack Bijuro alisema kabla ya kupata vitendea kazi ufanisi wa kazi katika shamba hilo ulikuwa unasuasua.

“Baadhi ya shughuli zikiwemo za ukaguzi wa shamba zilikuwa zinafanywa na watumishi waliokuwa wakilazimika kutembea kwa miguu sehemu moja hadi nyingine,” alisema.

Bijuro alisema kununuliwa kwa vifaa hivyo kutasaidia kuimarisha usimamizi wa shughuli zote za shamba na hivyo kuongeza ufanisi na tija kwa maendeleo ya Taifa.

Alivitaja vifaa hivyo na thamani yake kwenye mabano alisema greda (561,387,750), kijiko (561,387,750), Isuzu lori (206,265,600), Nissan Patrol Pick Up single cabin 3 (271,033,347) na Nissan patron station wagon 2 (224,865,342).

Vingine ni Nissan patrol 4WD standard (128,184,107.99), pikipiki Honda 25 (167,073,750), bus Nissan diesel moja (272,518,349.72)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment