Thursday, 6 February 2014

MCHUNGAJI MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI, AACHIWA KWA DHAMANA NI KUTOKANA NA KESI YA KUJERIHI


Akitoka mahabusu ya mahakama hiyo
Akiwasalimu wafuasi wake

Ndani ya mahakama

Akiteta na wakili wake Lwezaula Kaijage

Chiku Abwao (MB) baada ya kumdhamini akitoka katika mahakama hiyo

Akisalimia wafuasi wake baada ya kutoka mahakamani kwa dhamana

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) jana amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alisema Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli, mjini Iringa.

Alisema Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita kinyume na kifungu kidogo namba 225 cha sheria ya kanuni za adhabu.

Akiwa amefunguliwa kesi ya jinai namba 28 ya mwaka 2014, Mchungaji Msigwa anayetetewa na wakili Lwezaula Kaijage alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha kesi hiyo itakayotajwa tena Machi 10, mwaka huu kwa kile kilichoelezwa kwamba uchunguzi wake haujakamilika.

Pamoja na Mchungaji Msigwa, jeshi la Polisi limewapandisha kizimbani Meshack Chonanga (22) na Paulo Mapunda wote wakazi wa kijiji cha Nduli mjini Iringa  wakituhumiwa kumjeruhi Alex Mpiluka wakati wa kampeni hizo.

Watuhumiwa hao walirudisha mahabusu ya mahakama hiyo baada ya wadhamini wao kuchelewa kufika mahakamani hapo.

Kama ilivyokuwa kwa Mchungaji Msigwa, nao kila mmoja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana ya ahadi ya Sh Milioni 2.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment