Saturday, 8 February 2014

LEO NDIO LEO KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA KALENGA, WAGOMBEA TISA KUJINADI KWA WAJUMBE

LEO NDIO LEO kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  na wananchi wa jimbo la Kalenga wanaohitaji muwakilishi mpya.

Zaidi ya wajumbe 500 wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo hilo la Kalenga wanatarajia kuwawakilisha wana CCM wenzao kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Kalenga.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 4.30 asubuhi hii ya leo katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa na wajumbe wengi wameshawasili wakitokea kata 13 za jimbo hilo.

Kwa mujinu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka, uchaguzi wa kumpata mbunge atakayerithi viatu vya marehemu Dk William Mgimwa utafanyika, Machi 16, mwaka huu.

Kisaka amesema fomu za uteuzi kwa ajili ya wagombea wa vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo zitatolewa Februari 9 hadi 18.

Amesema uteuzi wa wagombea utafanyika Februari 18 na kampeni za uchaguzi zitaanza februari 19 hadi Machi 15.

WanaCCM wanaoshiriki kura hizo za maoni ni pamoja na Jackson Kiswaga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Tigo kanda ya Kusini.

Wengine ni mtoto wa marehemu Dk Williama Mgimwa, Godfrey Mgimwa, Mkuu wa Wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa, Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kisaba, Msafiri Pagamila na Thomas Mwakoka.

Tofauti na ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi, kabla ya kura hizo za maoni baadhi ya wagombe walikutwa katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mwembetogwa wakifuraji kwa pamoja.

Kila mmoja ameonesha matumaini ya kushinda kura hizo wakati wakiingoea na mtandao huu.
 
Jackson Kiswaga anavyoonekana asubuhi ya leo kabla ya kura za maoni


Kiswaga, msomi mwenye shahada ya biashara, kasema endapo atachaguliwa, atahakikisha anaipeperusha vyema bendera ya chama hicho huku akionesha matumaini makubwa ya CCM kutetetea kiti hicho.

“CCM ni chama chenye wafuasi wengi, sio tu Kalenga bali ni nchi nzima, kwahiyo yoyote atakayesimamishwa tutaamuunga mkono ili tupate ule ushindi wa kishindo,” alisema.

Anasema anazo ajenda na vipaumbele vingi vitakavyoharakisha maendeleo ya wana Kalenga kwakuwa ana fahamu changamoto zao.
Mama Mtasiwa kabla ya kura za maoni, asubuhi ya hii leo
 Mama Mtasiwa, mwenye shahada pia, alisema “naingia katika kinyang’anyiro hicho kwa mara ya pili sasa, nina matumaini makubwa ya kushinda. Kumbuka katika kura za maoni za 2010 nilikuwa mshindi wa tatu baada ya Dk Mgimwa na Abbas kandoro,” alisema.

Alisema anautegemea mtaji uliomuwezesha kushika nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro hicho kumuibua mshindi katika kura za maoni za leo.

Thomas Mwakoka mwalimu anayetafuta PHD alisema anayo nafasi ya kushinda katika kura hizo ili aendelele jimbo la kalenga, hata hivyo hiyo haitamzuia kumsaidia mgombea yoyote kutoka ndani ya chama chake atakayeibuka kidedea.

Thomas Mwakoka
Edward Mtakimo , mwalimu ngazi ya cheti, alisema hii ni mara yake ya pili katika kinyang’anyiro hicho. Anataka kutumia fani yake ya ualimu kuhakikisha jimbo la Kalenga linapiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo

Edward Mtakimo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment