Saturday, 8 February 2014

KUNA SHIDA YA MAJI IRINGA? HAPANA HAYA SIO MAJI NI KINYWAJI CHA ASILI KIKISAMBAZWA

Mfanyabishara wa pombe aina ya Ulanzi, akimuuzia mteja wake hii leo kama alivyokutwa na kamre yetu

Mteja anaonekana akiuhakiki kama haujachangwa na maji- mwishowe alisikika akisema huu ni mtogwa, hauleweshi haraka mpaka ulale siku moja, ukilala unabadilika toka Mtogwa na kuwa mkangafu

Ulanzi ni pombe maarufu inayotumiwa na wenyeji wa mkoa wa Iringa. Pombe hii hugemwa kutoka kwenye miti aina ya mianzi.

Ni pombe inayoolezwa na wanywaji kuchangia sasa kuongeza nguvu za kiume; watu wanaojifanya wana hadhi lakini wenye wanadaiwa kununua aina hii ya pombe kwa kuwatumia wafanyakazi wao na kuitumia kwa makusudi hayo ya kuongeza nguvu za kiume.

Huu ndio msimu wake mkuu; na katika msimu huu taarifa zinaeleza kwamba ngono zembe hufanyika sana hali inayochangia maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Mkoa wa Iringa ni wa pili kitaifa kwa kuwa na kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Wakiipenda pombe hiyo, wadau wameitaka idara ya Afya ya Manispaa ya Iringa kuwapatia elimu ya usafi pamoja na mazingira bora ya ugemaji ili iweze kuwa katika mazingira yatakayo boresha afya za watumiaji.
 
Wagemaji  na wasafirishaji wanatakiwa kupewa elimu ya usafi wakati wa kugema na utunzaji na usafishaji wa vyombo vinavyotumika kugemea na kusafirishia, alisema Mohamed Tall.

Baadhi  ya wakaazi wa manispaa ya Iringa wamelaani vikali kitendo  cha wauza ulanzi kutoka Tanangozi,Ihemi, Ifunda na sehemu nyingine kunywa ulanzi kupitia mrija wa mpira kutoka kwenye dumu hadi kinywani kwa mtumiaji bila kujali kuwa mate yanaweza kuingia  ndani kinywaji hicho na kuhatarisha maabukizo ya magonjwa kwa watumiaji wengine.
 
Tabia nyingine ambayo wadau hao walionesha kutoifumbia macho ni pamoja na mavazi machafu ambayo watu wanaosafirisha ulanzi huvaa pamoja na kuwa vyombo kama madumu  kutooshwa vizuri.

Waliongeza kuwa kukosekana na uangalizi mzuri wa mazingira mazima ya usafi kwa bidhaa hiyo kuwa kunaweza kuleta mlipuko wa magonjwa ambukizi yakiwemo ya Kifua Kikuu ( TB).
 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment