Tuesday, 11 February 2014

GODFREY MGIMWA, MTOTO WA DK MGIMWA ATEULIWA RASMI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM JIMBO LA KALENGA


Nape akimtambulisha Godfrey kwa waandishi wa habari, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.

Akizungumza na waandfishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Kamati Kuu ya CCM  imemridhia Godfrey kupeperusha bendera ya CCM baada ya kukidhi vigezo licha ya kuongoza katika kura za maoni jimboni humo.

Godfrey ni Mtoto wa tatu wa Marehemu Dk William Mgimwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga na Waziri wa Fedha kabla ya kifo chake Januari 1, mwaka huu.

Wakati wa mazishi ya baba yake katika kijiji Magunga, Godfrey alitoa salamu kwa niaba ya familia ya Dk William Mgimwa.

Na katika salamu zake alisema anao wosia alioachiwa na marehemu baba yake kabla ya kifo chake.

Wosia huo ulihusu ahadi alizotoa na kuzitekeleza kwa wananchi wa jimbo lake la Kalenga na akaomba serikali izibebe zile ambazo hazijatekelezwa ili izimalizie.

Kazi hizo ni pamoja na kusomesha watoto yatima, ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari, ujenzi wa miundombinu na mawasiliano, misaada kwa vikundi vya ujasriamali, na mkazo katika huduma za jamii ikiwemo afya, kilimo, na maji.

Alisema siku kumi kabla ya kifo cha baba yake, alimwambia ameandaa mabati 120 anayotaka kuyagawa katika maeneo mbalimbali jimboni mwaka kwa lengo la kusukuma maendeleo.

Kama atashinda kiti hicho, CCM na wananchi wa jimbo la Kalenga wanategemea mtoto huyo wa marehemu atamalizia kazi iliyobakizwa na marehemu baba yake.

Katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Godfrey Mgimwa anatarajiwa kumenyana na mmoja kati ya wanachama 13 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliojitokeza kusaka tiketi ya chama hicho kuwania jimbo hilo.

Mbali na muuza magazeti maarufu wa mjini Iringa, Aidan Pugili wengine waliojitokeza ni

Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema Makoga,  Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Mussa Mdede, Mchungaji Samweli  Nyakunga,  Daniel Luvanga, Anicent Sambala na Vitus Lawa .

Reactions:

0 comments:

Post a Comment