Kati
ya tarehe 13/02/2014 na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao
kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.
Vikao
hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya
Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.
Waliohojiwa
katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-
1. Ndg.
Frederick Sumaye
2. Ndugu
Edward Lowasa
3. Ndugu
Bernard Membe
4. Ndugu
Stephen Wassira
5. Ndugu
January Makamba
6. Ndugu
William Ngeleja
Baada
ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo
kupendekeza adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti
na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.
Kwa
ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-
1. Walithibitika
kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na
Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
2. Wamethibitika
kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya
vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu
wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za
kanuni hizo.
Kamati
Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu
ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo
wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi.
Tafsiri
ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo
la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:-
“Mwanachama
aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda
usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.”
Kamati
Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa
wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa
vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.
Aidha,
Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka
kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka
maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.
Imetolewa
na:-
Nape
Moses Nnauye,
KATIBU
WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI
NA UENEZI,
0 comments:
Post a Comment