Wednesday, 26 February 2014

CCM NA CHADEMA WAENDELEA NA KAMPENI ZAO KALENGA

Mgimwa akionesha utiifu kwa kusalimiana kimila na wazee wa jimbo hilo
MGOMBEA ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa leo ameendelea na mikutano yake ya kampeni katika kata ya Magulilwa.

Amefanya mikutano mitatu katika vijiji tofauti vya kata hiyo huku akiwasihi wananchi wa jimbo hilo kutofanya makosa katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika Machi 6, mwaka huu.

Mgimwa amesema anazijua changamoto za jimbo hilo na amejizatiti kikamilifu kushirikiana na wananchi kuzipatia ufumbuzi.

Naye Grace Tendega anayetafuta nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa fursa ya kuwatumikia.

katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Tanangozi hii leo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amewaangukia wananchi wa kijiji hicho akiwaomba wamchague Tendega ili akaongze nguvu ya wabunge wa Chadema katika bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment