Tuesday, 4 February 2014

BWENI LA WAVULANA SEKONDARI YA NJOMBE LATEKETEA KWA MOTO

Jitihada za kuuzima moto huo zilivyokuwa
BWENI la wavulana wa shule ya sekondari Njombe mkoani Njombe limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Njombe, Fulgency Ngonyani amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme iliyotokea katika bweni hilo.

Alisema bweni hilo lilikuwa likitumiwa na wanafunzi 42 wa kidato cha tano na sita.

Alizitaja baadhi ya mali zilizotekea kwa moto huo kuwa ni pamoja na vitanda, magodoro, mabegi ya nguo na nguo zilizokuwemo, masunduku ya vitabu na fedha taslimu.

Pamoja na kuteketeza mali hizo, moto huo haukumdhuru mwanafunzi hata mmoja kwani ulipoanza kuwaka wengi wao hawakuwepo bwenini.

Uongozi wa shule hiyome umekadiri hasa iliyotokana na moto huo kuwa zaidi ya Sh Milioni 63.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment