Wednesday, 5 February 2014

BREAKING NEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEWS- WAFUASI WA CHADEMA WAKAMATWA NA POLISI WAKINUNUA SHAHADA ZA WAPIGA KURA KATA YA NDULI

mgombea udiwani kata ya Nduli kupitia Chadema akiwa katika moja ya mikutano yake pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa wapshaji wetu habari walioko kata ya Nduli Iringa Mjini ambako kampeni za uchaguzi mdogo zinaendelea zinadai kwamba baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekamatwa na Polisi wakinunua shahada za wapiga kura.

Imeelezwa na wapashaji hao kwamba wafuasi hao walikamatwa leo asubuhi wakinunua shahada za wapiga kura kutoka kwa wafuasi wanaoaminika kuwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi hakuweza kupatikana mara kuthibitisha taarifa hizo (tunaendelea kumtafuta), hata hivyo Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Ndio tumepata taarifa hizo mapema hii leo kwamba kuna wafuasi wa Chadema wamekamatwa wakinunua shahada za wapiga kura wetu," alisema.

Alisema taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo wanasubiri kutoka jeshi la Polisi ili nao wajue hatua za kuchukua.

Tukio hilo limetokea zikiwa zimebaki siku tatu tu za kampeni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao kinyang'anyiro chake ni kati ya mgombea wa CCM, Bashiri Mtove na wa Chadema Ayubu Mwenda.

Uchaguzi huo utafanyika Februari 9, mwaka huu sambamba na kata zingine 26 nchini kote ambazo waliokuwa madiwani wake kwasababu mbalimbali ikiwemo ya kifo walizifanya ziwe wazi. 

Reactions:

1 comments:

  1. If you want to find more information how Dermatology in delhi can benefit you then you can visit Dermatologist in delhi

    ReplyDelete