Wednesday, 5 February 2014

ATAKAYEFICHUA WAKWEPA KODI KUZAWADIWA MILIONI 20

Tanzania Revenue Authority

MAMLAKA ya Mapato (TRA) imeamua mtu atakayefichua wakwepa kodi kwa kutaja majina, atazawadia kitita cha Sh Milioni 20.

Hayo yalisemwa na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Patrick Kasera kwa nyakati tofauti alipokuwa jijini Mwanza na Musoma katika msafara wa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa.

"Waleteni watu wanaokwepa kulipa kodi ili mtajirike," alisema na kuongeza kwamba atakayefanya hivyo atazawadia kiasi hicho cha fedha bila kutajwa jina lake hadharani.

Wakati huo huo alitoa ufafanuzi juu ya bei za Mshine za Kodi za Kielekroniki (EFDs), kwa wafanyabishara kurahisisha ulipaji wa kodi na kufanya biashara yenye tija na ubora nchini.

Kasera alisema bei ya chini ya sasa ya mshine za EFD ni Sh 600,000 na ya juu ni Sh 690,000 kiasi hicho kikijumuisha gharama za usafirishaji.

"Serikali haifanyi biashara ya kuwaumiza, kuwanyanyasa na kuwaonea na hakuna faida yoyote inayopata inapofanya hivyo kwa watu wake.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment