Thursday, 30 January 2014

LIGI SOKA YANUKIA MJINI IRINGA, MSHINDI WA KWANZA KUTOKA NA MILIONI MOJA

Nuru Hepautwa kuanzisha ligi soka mjini Iringa

LIGI mpya ya mpira wa miguu inayotarajiwa kuvuta hisia za wakazi wengi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake itaanza kutimua vumbo Machi 14 katika viwanja vya Samora na Kleruu, mjini hapa.

Ligi hiyo iliyopewa jina la Hepautwa Cup itashirikisha timu 16 kutoka kata 16 za manispaa ya Iringa.

Mfadhili wa ligi hiyo itakayokuwa ikichezwa kila mwaka kwa miezi mitatu mfululizo, Nuru Hepautwa alisema jana kwamba mshindi wa kwanza atakuwa kiondoka na Sh Milioni moja na zawadi nyingine mbalimbali.

“Mshindi wa Pili atajinyakulia Sh 500,000 na wa tatu Sh 200,000,” alisema na kusisitiza kwamba lengo lake ni kuona ligo hiyo inasukuma mbele gurudumu la mchezo wa soka mkoani hapa.

Alisema inasikitisha kuona kwamba timu wachezaji wengi wanacheza timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza wanatoka nje ya mkoa wa Iringa.

Akiuliza kwanini Iringa iendelee kutegemea vipaji kutoka nje ya mkoa wa Iringa, Hepautwa alisema “muda umefika wa kuwa na ligi yenye tija na itakayohamsisha wanyeji wa mkoa wa Iringa na wadau wake kuwekeza zaidi kwenye mchezo huo.”

Alisema mbali na zawadi hizo kila timu itakayoshiriki ligi hiyo itapewa seti moja ya jezi, mipira na vifaa vingine vya mchezo huo.

Hepautwa ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa anayefanya biashara zake jijini Dar es Salaam alisema muda kubadili soka la mkoa wa Iringa umefika.

“Ni matarajio yangu Hepautwa Cup itachochea vijana wetu kuupenda mchezo wa soka na hatimaye tupate vijana watakajiunga na timu zetu zinazoshiriki ligi mbalimbali za juu ikiwemo Lipuli,” alisema.

Kwa mara ya mwisho kwa wakazi wa mkoa wa Iringa kushuhudia ligi kuu ikichezwa mkoani hapa ni mwaka 1999 kabla timu ya Lipuli haijashuka daraja na jitihada zake za kurudi kwenye ligo hiyo zikiendelea kugonga mwamba mwaka hadi mwaka.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment