Wednesday, 22 January 2014

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED

Juan Mata

Kiungo wa klabu ya Chelsea Juan Mata anaelekea kukimbilia klabu ya Manchester United mwishoni mwa wiki hii katika usajili unaotarajiwa kuiingiza Chelsea zaidi ya Pauni za Kingereza Milioni 37.

Hata hivyo Gary Neville, beki wa zamani ya ManU ameponda mpango wa klabu hiyo wa kumsajili mchezaji huyo kwa dau hilo akisema halilingani na uwezo wake.

"Ni kwasababu wanataka kusajili damu mpya, lakini siamini kama dau hilo linalingana na mchezaji huo na siamini pia kama atafiti kwenye mipango na falsafa ya Manchester United, kama ningeulizwa ningezema Hapana," Neville anasema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment